KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, February 14, 2011

Mama Sidibe NJE MSIMU MZIMA !!!


Ndoto wa mshambuliaji wa klabu ya Stoke city Mamady Sidibe, za kuisaidia timu ya taifa lake la Mali katika harakati za kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika zimeingia gizani baada ya kuumia kisigino mwishoni mwa juma lililopita.

Mshambuliaji huyo aliekua mstari wa mbele kuhakikisha nchi yake inatinga katika fainali hizo zitakazochezwa nchini Equatorial Guinea pamoja na Benin amefikwa na maswahibu ya kuumia kisigono alipokua kwenye jukumu la kuitumikia klabu yake ambayo ilifunga safari hadi St Andrews kucheza na wenyeji Birmingham City katika michuano ya ligi ya nchini Uingereza.

Taarifa za mchezaji huyo kuumia zimetolewa na meneja wa klabu ya Stoke City, Tonny Richard Pulis wakati akizungumza na waandishi wa habari huko Britania Stadium mara baada ya kupokea taarifa kamili kutoka kwenye jopo la madaktari wa klabu hiyo.

Pulis amesema Mamady Sidibe mwenye umri wa miaka 31, amefanyiwa vipimo na amethibitika kuumia vibaya sehemu za kisigino cha mkuu wake wa kulia hivyo itamchukua muda wa miezi sita ijayo kuwa nje ya uwanja.

Hii si mara ya kwanza kwa Mamady Sidibe kuumia sehemu hiyo, kwani kama itakumbukwa vyema msimu uliopita mshambuliaji huyo aliumia kisigino na kujikuta akishauriwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha msimu mzima kabla ya kurejea tena mwanzoni mwa msimu huu.

Kufuatia taarifa hizo uongozi wa shirikisho la soka nchini Mali umetoa kauli ya kusikitishwa na hatua ya kuumia kwa mshambuliaji huyo ambae hata hivyo wamemtakia kila la kheri ili aweze kurejea mapema uwanjani.

No comments:

Post a Comment