
Ligi kuu ya soka nchini Uingereza hii leo inaendelea tena kwa mchezo mmoja kuchezwa huko Craven Cottage ambapo mabingwa watetezi Chelsea watafanya safari ya kuwatembelea majirani zao Fulham Fc.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na kila aina ya ushindani kutokana na pande zote mbili kuwa na malengo yanayotaka kufanana ambapo kwa upande wa Fulham Fc, wao dhamira yao ni kutaka kusaka ushindi na kufuta makosa waliyoyafanya katika mchezo uliopita dhidi ya Aston Villa ambao walilazimisha sare wa mabao mawili kwa mawili.
Meneja wa klabu ya Fulham Leslie Mark Hughes amesema usiku huu watakwenda katika uwanja wao wa nyumbani lengo likiwa ni moja tu la kutotaka kurejea makosa walioyoyafanya katika michezo ilioyopita na ana amini kikosi chake kina uwezo mkubwa wa kufanya hivyo.

Nae meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Michelangelo Ancelotti amesema kila mmoja wao anatambua nini umuhimu wa mchezo wa hii leo na tayari ameshawambia wachezaji wake kwa ujumla kusahau suala la ubingwa na badala yake wafikiria michezo inayowakabili kwa sasa wakianza na mchezo wa usiku huu.
Hata hivyo meneja huyo wa kiamataifa toka nchini Italia akaguzia suala la kupata wakati mgumu wa kuwazoesha washambuliaji wake kucheza kwa pamoja baada ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Hispania Fernando José Torres Sanz.
Amesema lengo la kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ni kutaka kufanya utaratibu wa kuwachezesha kwa zamu wachezaji wake wanaoitumikuia safu ya upachikaji mabao.
No comments:
Post a Comment