
Meneja wa klabu ya Fulham Leslie Mark Hughes amesema hakufurahishwa na kitendo alichofanyiwa na meneja wa klabu ya Man city Roberto Mancini mara baada ya mchezo wa jana kumalizika huko City Of Manchester.
Leslie Mark Hughes amesema kitendo cha meneja wa klabu ya Man city kumpa mkono huku akishindwa kumtazama usoni kilimchukiza hadi kufikia hatua ya kumuona ni mtu mbinafsi na asiependa kumuona machoni mwake.
Amesema si mara ya kwanza kwa meneja huyo kufanya kitendo hicho kwani hata alipozulu Craven Cottage alifanya hivyo mara baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa.
Leslie Mark Hughes ambae jana alirejea City of Manchester akiwa kama meneja wa klabu pinzani ameongeza kwamba Roberto Mancini amekua na tabia za dharau ambazo haziwezi kuvumiliwa na yoyote yule.
Katika hatua nyingine meneja huyo wa kimataifa toka nchini Wales ameonyesha kufurahishwa na matokeo ya sare yaliyopatikana katika mchezo huo ambao ulishuhudia wakienda mapumziko wakiwa nyuma kwa idadi ya bao moja kwa sifuri lililofungwa na Super Mario Balotelli.
Hughes amesema alitumia muda wa mapumziko vyema kwa kuawaasa wachezaji wake kucheza kwa ukakamavu na juhudi ambazo hata hivyo zilisawaidia na mwisho wa dakika tisini walijikuta wanaondoka uwnajani hapo wakigawana point na wenyeji wao kufutia bao lililofungwa na Damian Duff.
Roberto Mancini meneja wa klabu ya Man City baada ya matokeo hayo ya bao moja kwa moja ametoa kisingizo cha uchovu uwanaowakabili wachezaji wake kutokana na ratiba ya ligi

Amesema ni vigumu kwa mchezaji wa kawaida kucheza kila baada ya siku tatu hivyo inamlazimu kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wake muhimu ambao anaamini endapo wangejumuika na baadhi ya wachezaji wengine katika mchezo huo walikua na kila sababu ya kuzibakisha point tatu nyumbani.
No comments:
Post a Comment