
Baada ya kushindwa kutimiza malengo ya kurejesha heshima iliyopitea huko Emirates kwa muda wa miaka sita iliyopita kwa kutwaa ubingwa wa michuano yoyote wanayoshiriki, meneja wa klabu y Arsenal Arsene Charles Ernast Wenger amewataka wachezaji wake kusahau yaliyopita na kutazama kilicho mbele yao.
Arsene Charles Ernast Wenger amewataka wachezaji wake kuwa katika mfumo huo kwa lengo la kutojiharibia mikakati waliyojiwekea msimu huu ya kuhakikisha wanamaliza ukame wa vikombe ambao huenda ukaisha kutokana na mwenendo mzuri walionao kwenye michuano wanayoendelea kushiriki.
Amesema ni wakati mwingine wa kufungua ukurasa mpya wa kuendelea kupambana mara baada ya kufungwa katika mchezo wa jana wa hatua ya fainali wa michuano ya kombe la ligi hivyo haoni sababu kwa yoyote alie sambamba na yeye kukatishwa tamaa na matokeo hayo.
Amesema kiujumla hawakustahili kufungwa katika mchezo huo lakini makosa yaliyojitokeza dakika za lala salama, kufuatia kujichanganya kwa beki Laurent Koscielny dhidi ya kipa Wojciech Szczesny na kumpa mwanya Obafemi Martins kufunga bao la ushindi kirahisi walilazimika kukubaliana na matokeo ambayo katu hayatobadilika katika historia ya soka.
Hata hivyo mzee huyo mwenye umri wa miaka 61 amekiri kwamba kufungwa katika mchezo muhimu kama wa jana inaumiza lakini hawana budi kuhimizana kuanza mikakati tofauti ya kuhakikisha msimu huu wanaendelea kusaka mafanikio zaidi.
Amesema kwa sasa wanaanza maandalizi ya mchezo wa marejeano wa hatua ya tano ya kombe la ligi dhidi ya Leyton Orient utakaochezwa Emirates Stadium siku ya Jumatano na imani yake yamtuma kikosi chake kitafanya vyema na kutinga katika hatua ya robo fainali ambapo watacheza na Manchester United.
Pia akaanisha kwamba maandalizi ya mchezo huo wa jumatano yanakwenda sambamba na mchezo wa ligi utakaochezwa mwishoni mwa juma hili huko jijini London ambapo Sunderland watazulu Emirates kwa madhumuni ya kusaka point tatu muhimu.
No comments:
Post a Comment