
Baada ya kisago cha mabao mawili kwa moja kilichotolewa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya mahasimu wake wakubwa Man Utd, meneja wa klabu ya Man city Roberto Mancini amekiri kuanza kuona mambo magumu katika harakati za kutwaa ubingwa msimu huu.
Roberto Mancini aliekua na jeuri ya kutwaa ubingwa toka mwanzoni mwa msimu huu, huku akijidaia kikosi chake kilichosheheni wachezaji wa gharama kubwa amesema katika mazingira ya kawaida hana budi kujiondoa katika mbio hizo kutokana na ugumu unaomkabili kwa sasa.
Amesema kupoteza point tatu muhimu katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Man Utd ni kosa kubwa sana kwa upande wake ambalo linamuweka njia panda ya kujiuliza ni vipi atakavyoanza mikakati ya kushinda michezo iliyosalia huku akiwaombea mabaya wapinzani wake.
Amesema kimahesabu michezo iliyuosalia ni 11 kabla ya msimu wa mwaka 2010-11 haujamalizika na mpaka sasa wapo nyuma kwa tofauti ya point 8 dhidi ya Man utd, hivyo wana kazi ya ziada ya kufanya, katika ligi hiyo sambamba na kwenye michuano ya ligi ya soka barani Ulaya.
Wakati Mancini akijutia kupoteza nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu, mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza pamoja na klabu ya Man Utd, Wayne Rooney ameendelea kutamba kufutia bao alilofunga mwishoni mwa juma lililopita na kuizawadia ushindi klabu yake dhidi ya mahasimu wao wakubwa Man City.
Amesema ni bao zuri kwa kila mmoja kwa kulikubali machoni na moyoni pia na daima litaendelea kuwepo katika kumbu kumbu za mabao matano aliyoifungia klabu yake dhidi ya Man City toka aliposajiliwa huko Old Trafford mwaka 2004.Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ameendelea kusisitiza kwamba licha ya kufurahishwa na hatua ya ufungaji, bado bao hilo linampa nafasi nyingine ya kujisifia kwani ndio bao pekee lililoiondosha Man city katika mbio za ubingwa msimu huu.
Wakati Mancini akionyesha kukatishwa tamaa na mwenendo wa kikosi chake, meneja wa klabu ya Arsenal Arsène Charles Ernest Wenger ameendelea kutangaza vita ya kuusaka ubingwa wa msimu huu mpaka kitakapo eleweka dhidi ya wapinzani wake.
Wenger ambae alikishuhudia kikosi chake kikiibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri mbele ya fupa lililomshinda Man Utd Wolves Hampton Wanderres amesema ushindi wao wa mwishoni mwa juma lililopita umeendelea kuwaweka katika mazingira mazuri ya kuendelea kufikiria mazuri msimu huu hivyo inamlazimu kutangaza vita hiyo.
Amesema hakuna linaloshindikana kwa hivi sasa, kwani bado ana kikosi kizuri na chenye kuweza ushindani katika kila mchezo ulio mbele yao.Kwa hivi sasa Man Utd ndio wapo kileleni kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha point 57, wakifuatiwa na Arsenal wenye point 53 na Man City wanakamata nafasi ya tatu kwa kuwa na point 49.
No comments:
Post a Comment