
Mshambuliaji Fernando Torres amepasua ukweli kwa kueleza kwamba mpaka hii leo hajawahi kukutana na bosi wa ngazi ya juu wa klabu hiyo Roman Abramovich licha ya kusajiliwa kwa fedha nyingi akitokea Liverpool mwishoni mwa mwezi uliopita.
Torres amesema ukweli huo baada ya kuhojiwa na vyombo vya habari vya mjini London ambapo amebaisha kwamba ameshangazwa na hatua hiyo ambapo yeye binafsi alidhani huenda ingekua rahisi kuonana na kibopa huyo wa kirusi ambae ana hakika alifurahishwa na kukubali kwake kujiunga na The Blues.
Amesema licha ya kutokuwepo kwa mawasiliano kati yake na mkuu huyo bado anajihisi mwenye furaha na anaamini ipo siku atakutana nae na kubadilishana nae mawazo.
No comments:
Post a Comment