
Beki wa kimataifa toka nchini Ufaransa Bacary Sagna ameeleza kuwa alijisikia aibu baada ya klabu yake kupoteza mchezo muhimu wa hatua ya fainali ya kombe la ligi *Curling Cup* hapo jana dhidi ya Birmingham City.
Bacary Sagna ametoa maelezo hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamiii wa Twiter huku akiwataka radhi mashabiki wa klabu ya Arsenal ambao walikua wakisubiri kutimiza ndoto za kufuta mawazo machafu ya kushindwa kutwaa ubingwa kwa muda wa miaka sita iliyopita.
Katika maelezo yake Sagna ameandika kwamba ni aibu kubwa kwake kuona wameshindwa kutimiza lengo waliklo likusudia katika michuano hiyo hivyo hawana jinsi ya kujitahidi kadri wanavyoweza kuhakikisha wanafanya vyema katika michuano mingine wanayoendelea kushiriki.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 28, ameendelea kubainisha kwamba kilichomuuza sana hadi kufikia hatua ya kujihisi aibu ni kitendo cha kuwa karibu makosa yaliyowagharimu katika dakika za mwisho kutokana na muingiliano uliofanywa na beki Laurent Koscielny pamoja na Wojciech Szczesny katika dakika ya 89 na kutoa mwanya kwa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Nigeria Obafemi Martins kufunga bao la ushindi kirahisi.
Wachezaji wengine walioomba radhi kupitia mtandao huo wa kijamiii ni:
Jack Wilshere, ambae alifanikiwa kucheza kwa kujituma wakati wote ambapo yeye katika ukurasa wake ameandika kwamba ameumizwa sana na kitendo cha kupoteza mchezo huo muhimu lakini akawataka radhi mashabiki huku akiwaomba kuendelea kushikamana na kukiamini kikosi chao ambacho bado kinaendelea kupigana kwenye michuano ya aina tatu tofauti.
Robin van Persie, yeye akaandika kwamba ni vigumu kuamini kama kweli wamepoteza lakini ukweli ndio huo ila bado na yeye akaomba radhi kwa mashabiki kwa kushindwa kurejesha ubingwa wa kombe la ligi kaskazini mwa jiji la London ambapo kwa mara ya mwisho ulinyakuliwa na Man utd ukitokea kwa Tottenham Hotspurs.
Nahodha na kiungo wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas yeye hakusita kukipa tano kikosi cha Birmingham City kwa kueleza ni kizuri na kimefanya kazi ya kutumia makosa waliyoyafanya.
Cesc Fabregas pia akawashukuru mashabiki wa The Gunners kwa mshikamano wao wanaendelea kuwaonyesha mpaka sasa hivi.
No comments:
Post a Comment