KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, February 28, 2011

Daniel Andre "Danny" Sturridge KUSABABISHA VITA.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza Daniel Andre "Danny" Sturridge mwishoni mwa msimu huu huenda akazusha vita kubwa kati ya meneja wa klabu ya Bolton Wanderers Owen Columba Coyle dhidi ya meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Michelangelo Ancelotti.

Vita inayohofiwa huenda ikasababishwa na mshambuliaji huyo ni harakati za kusajiliwa moja kwa moja ndani ya klabu ay Bolton Wanderers ambayo kwa sasa anaitumikia kwa mkopo baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea ambacho kimesheheni washambuliaji wengi na wazuri.

Tayari meneja wa klabu ya Bolton Wanderers Owen Columba Coyle ameshatangaza kuwa tayari kutuma ofa huko Stamford Bridge ya kutka kumsajilki mshambuliji huyo moja kwa moja baada ya kuridhishwa na kiwango chake toka alipomsajili kwa mkopo mwezi januari mwaka huu.

Amesema anafurahishwa na maendeleo ya Daniel Andre "Danny" Sturridge ambae tayari ameshaifungia klabu hiyo mabao manne ndani ya michezo minne aliyocheza.

Kwa upande wa meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Michelangelo Ancelotti nae ameshatoa msimamo wake wa kutokua tayari kumuuza mshambuliaji huyo kufuatia kuwepo kwenye mipango yake ya baadae mara tu atakapo maliza mkataba wake wa mkopo huko Reebok Stadium.

No comments:

Post a Comment