
Juma moja baada ya kutimuliwa kazi huko nchini Ujerumani kwenye klabu ya VfL Wolfsburg meneja wa kimataifa toka nchini Uingereza Stephen Steve McClaren ameeleza wazi dhamira yake ya kuwa tayari kufanya kazi na yoyote yule kwa hivi sasa.
Stephen Steve McClaren ambae kwa sasa yupo nyumbani kwao Uingereza baada ya kufungasha virago vyake huko nchini Ujerumani, amesema yoyote atakaejitokeza kwa sasa atakua tayari kufanya nae kazi lakini kwa makubaliano maalum ambayo yatamnufaisha kila mmoja baina yao.
Amesema licha ya kueleza wazi kuwa tayari kufanya kazi na yoyote, lakini amebainisha kwamba itapendeza mno endapo atapata nafasi ya kuendeleza ujuzi wa ufundishaji wake ndani ya nchi yake ya Uingereza aidha iwe katika ligi kuu ama ligi daraja la kwanza.
Stephen Steve McClaren toka alipoondoka nyumbani kwao Uingereza mwaka 2008, amekua meneja aliejipatia mafanikio makubwa ya kuzisaidia klabu za nje ya nchi hiyo na kufiki hatua ya kuzipa ubingwa ambapo kwa mara ya kwanza alifanya hivyo akiwa na FC Twenty kwa kuipa ubingwa wa nchini Uholanzi katika msimu wa mwaka 2009-10.
Akiwa nchini Ujerumani alifanikiwa kuizawadia nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa VfL Wolfsburg katika msimu wa mwaka 2010-11.
No comments:
Post a Comment