
Jopo la madaktari wa klabu ya Arsenal likiongozwa na daktari mkuu wa kikosi cha klabu hiyo Colin Lewin limempa baraka zote Arsene Wenger za kumtumia kiungo wa kimataifa toka nchini Ufaransa Samir Nasri katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Fc Barcelona utakaopigwa kesho huko kaskazini mwa jiji la London.
Jopo hilo la madaktari limempa baraka hizo mzee huyo mwenye umri wa miaka 61, baada ya kumfanyia vipimo Samir Nasri kwa mara ya mwisho hapo jana na amebainika ana uwezo wa kujumuishwa kikosini hiyo kesho.
Akitangaza kwenye mkutano wa waandishi wa habari Arsene Wenger amesema kiujumla kikosi chake kipo tayari kupambana na amefurahishwa na kurejea kwa Samir Nasri ambae alikua akiwaumiza vichwa kwa muda wa majuma mawili sasa kama angeweza kuuwahi mchezo huo muhimu.
Hata hivyo amesema bado hajafahamu kama atamuanzisha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 katika kikosi chake cha kwanza, lakini akasisitiza uwezekano wa kumtumia katika mpambano huo.
Kama itakumbukwa vyema Samir Nasri alikua akisumbuliwa na maumivu ya nyama za paja aliyoyapata kweye mchezo wa kombe la chama cha soka nchini Uingereza FA uliochezwa mwishoni mwa mwezi uliopita kati ya Arsenal dhidi ya Hudusfield Town.
No comments:
Post a Comment