KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 31, 2011

Robert David Keane AIHAMA SPURS.


Hatimae mshambuliaji wa kimataifa toka jamuhuri ya Ireland Robert David Keane amefanikisha safari ya kuondoka huko White Hert Lane, na kujiunga na wagonga nyundo wa London Wet Ham Utd wenye uchu wa kuhakikisha wanasalia katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu ujao.

Robie Kean ametimiza safari hiyo usiku wa kuamkia hii leo ambapo wagonga nyundo wamempata kwa mkopo na huenda wakamsajili moja kwa moja endapo watafanikiwa kusalia kwenye michuano ya ligi kuu msimu ujao.

Kabla ya kukamilika kwa usajili wake, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, alionekana huko upton Park akifuatiliwa mchezo wa kombe la FA ambapo West Ham Utd walikua wakicheza na Nottingham Forest ambao walikubali kisago cha mabao matatu kwa mawili.

Hata hivyo mara baada ya mchezo huo kumalizika, utaratibu wa usajili wa mshambuliaji huyo nao ukawa umemalizika na akapata nafasi ya kuzungumza na vyombo vya habari ambapo amesema ni furaha kubwa sana kwake ambapo anaamini uhamisho huo utamrejesha uwanjani baada ya kukaa benchi kwa muda mrefu.

Amesema jukumu lake kubwa kwa sasa ni kusaidiana na wachezaji wengine klabuni hapo na kuhakikisha West Ham Utd haishuki daraja msimu huu, kufuatia kuwa katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi mpaka hivi sasa.

Kwa upande wake meneja wa klabu ya West Ham Utd Avram Grant amesema kusajiliwa na mshambuliaji huyo ndani ya kikosi chake anaamini tatizo la umaliziaji ambalo mara kadhaa limekua likiwasumbua limepata ufumbuzi huku akimsifia Kean kwa kumuelezea atakavyo.

No comments:

Post a Comment