
Kiungo wa kimataifa toka nchini Ufaransa pamoja na klabu ya Arsenal Samir Nasri amejumuishwa kwenye kikosi kitakachowavaa mabingwa wa soka wa nchini Hispania Fc Barcelona katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya hapo kesho.
Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Charles Ernest Wenger amefanya maamuzi ya kumjumuisha kikosini kiungo huyo baada ya kupokea taarifa njema kutoka kwa jopo la madaktari wa klabu hiyo ambao wamekua wakimshughulikia Nasri kwa muda wa majuma mawili sasa.
Hata hivyo bado haijaelezwa kama kuna uwezekano kwa Samir Nasri kuanzishwa katika kikosi cha kwanza ama kusubiri kwenda kuchukua nafasi ya mnchezji mwingine pale mambo yatakapokua yameharibia.
Taarifa hizo zimeendelea kueleza kwamba kiungo wa kimataifa toka nchini Ufaransa pia Abou Diaby ameachwa kwenye kikosi hicho kufuatia maumivu wa kigimbi cha mguu yanayomsumbua toka aliporejea katika majukumu ya kitaifa huku kiungo wa kimataifa toka jamuhuri ya Czech Tomas Rosicky akirejeshwa kikosini baada ya kupona.
No comments:
Post a Comment