KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, February 15, 2011

UEFA CHAMPION LEAGUE KUENDELEA TENA HII LEO.


Baada ya kusimama kwa muda wa miezi miwili iliyiopita, ligi ya mabingwa barani ulaya usiku huu inaendelea tena kwa kushuhudia mwanzo wa hatua ya 16 bora ambayo inavishirikisha vilabu 16 vitakavyowania nafasi 8 za hatua ya robo fainali.

Michuano hiyo inaendelea usiku huu kwa michezo miwili ambayo itachezwa katika viwanja vya nchi mbili tofauti ambapo moja ya michezo hiyo ni ule kati ya Tottenham Hotspurs dhidi ya mabingwa wa zamani wa Ulaya Ac Milan watakaokua nyumbani huko Sun Siro mjini Milan.

Spurs wanacheza ugenini hii leo huku wakigubikwa na kumbu kumbu za kuutumia uwanja wa Sun Siro uliopo mjini Milan vizuri, ambao uliwaonyesha maajabu makubwa mashabiki wa soka mjini humo pale klabu hiyo ya jijini London ilipocheza na Inter Milan kwenye hatua ya kundi la kwanza na ambapo hadi katika muda wa mapumziko ilikua nyuma kwa idadi ya mabao manne kwa sifuri na katika kipindi cha pili al-manusura mabao hayo yarejeshwe yote lakini mpaka mwisho ubao wa mgoli ulisomeka mabao manne dhidi ya matatu.

Meneja wa klabu ya Tottenham Hotsopurs Harry Redknapp tayari ameshaeleza dhamira yao hii leo ya kupambana na AC Milan.

Dhamira hiyo iliyoelezwa wazi na meneja huyo ni ya kucheza kwa kushambulia wakati wote na si kujihami kama inavyokua kwa timu nyingi zinapokua ugenini ambapo amebainisha kwamba hatua hiyo ana imani itawasaidia kupata picha kamili ya mchezo ujao.

Nae nahodha wa kikosi cha Spurs William Gallas amesema hawana cha kuhofia usiku huu kwani wana imani wanakwenda kucheza na klabu inayowatambua vizuri kufuatia mabadiliko makubwa yaliyojitokeza ndani ya kikosi chao.

Amesema mara nyingi meneja wao amekua akiwajenga kisaikolojia na kuwahimiza kutoihofia timu yoyote wanayokutana nayo na wao hufanya kile wanachoelezwa hivyo hawana sababu ya kuwahofia AC Milan.

Historia yaonyesha kwamba klabu hizi zimeshawahi kukutana katika michuano ya kimataifa nah ii ilikua mwaka;

05-Apr-1972 Spurs 2-1 AC Milan

19-Apr-1972 AC Milan 1-1 Spurs

Mchezo mwingine wa hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya utakaochezwa hii leo utapigwa huko nchini Hispania katika uwanja wa Mestella ambapo wenyeji wa uwanja huo Vallencia watawakaribisha Shalke O4 kutoka nchini ujerumani.

No comments:

Post a Comment