
Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba amejiunga na wanamichezo wengine wanaomuunga mkono beki wan chi hiyo Habib Kolo Toure ambae amebainika kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni.
Didier Drogba ametangaza kuingia kwenye kampeni hiyo ya utetezi dhidi ya Habib Kolo Toure alipokua mjini Barcelona kwenye shughuli za taasisi ya kutetea haki za binaadamu kupitia michezo ambapo amesema alihuzinishwa sana na taarifa za mchezaji huyo kubainika anatumia dawa za kuongeza nguvu michezoni.
Amesema baada ya taarifa hizo kutolewa juma lililopita alifanya utaratibu wa kuzungumza na Habib Kolo Toure na kumuuliza kulikoni lakini maelezo aliyoyasikia kutoka kwake yanampa mwanya wa kujiunga na wanamichezo wengine waliotangaza kumtetea beki huyo mwenye umri wa miaka 29.
Wanamichezo ambao tayari wameshatangaza kuwa pamoja na Habib Kolo Toure katika kesi hiyo ni ndugu yake Yaya Toure sambamba na wachezaji wote wa klabu ya Man City, baba mzazi wa mchezaji huyo pamoja na meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger.

No comments:
Post a Comment