KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, March 11, 2011

Wolfgang-Felix Magath HAKUFIKA MAZOEZINI.


Siku moja baada ya kukanusha taarifa za kutokua mbioni kuondoka huko Veltins-Arena meneja wa klabu ya Schalke 04 Wolfgang-Felix Magath jana hakuonekana mazoezini hali ambayo imezua hofu upya kwa mashabiki wa klabu hiyo ya nchini Ujerumani.

Mashabiki waliohudhuria kwenye mazoezi ya kikosi chao baada ya kusonga mbele kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya walionekana kushangazwa na hatua hiyo huku meneja msaidizi akishindwa kusema lolote pale alipohitajika kuzungumzia suala hilo.

Hata hivyo licha ya kuwepo kwa hali hiyo bado mashabiki waliendelea kutazama mazoezi ya kikosi chao huku minong’ono ikitawala miongoni mwao ambapo baadhi ya mashabiki walionyesha kuwa na matumaini huenda jana haikua siku nzuri kwa Wolfgang-Felix Magath kufika uwanjani hapo.

Wolfgang-Felix Magath anahusishwa na taarifa za kuwa mbioni kuondoka klabuni hapo kufuatia kushindwa kufikia malengo yaliyowekwa na viongozi wa klabu hiyo ya kuhakikisha wanacheza michuano ya barani ulaya msimu ujao hali ambayo inaonekana kushindikana kwa sasa kufuatia nafasi waliopo kwenye msimamo wa ligi.

No comments:

Post a Comment