KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, March 1, 2011

Emmanuel Chinenye Emenike KUWAKABILI ETHIOPIA.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Nigeria pamoja na klabu ya Karabükspor ya nchini Uturuki Emmanuel Chinenye Emenike huenda akawa fit kabla ya mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika za mwaka 2012 dhidi ya timu ya taifa ya Ethiopia.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23anapewa nafasi kubwa ya kucheza mchezo huo kufuatia hali yake kuendelea vyema baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda wa majuma sita yaliyopita kutokana na maumivu ya goti yanayomkabili.

Sababu kubwa ya kupigiwa chepuo la kuingia kikosini na kuwakabili Ethiopia katika mchezo wa March 26, ni kutokana na kiwango chake kizuri ambacho kiliisaidia Nigeria katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa February 9 dhidi ya timu ya taifa ya Sierra Leone iliyokubalia kichapo cha mabao mawili kwa moja.

Emmanuel Chinenye Emenike amezungumza na vyombo mbali mbali vya nchini Nigeria na kuthibitisha kuwa anaendelea vyema na imani yake yamtuma huenda akawa tayari kabla ya March 26 siku ambayo itakua maalum kwa ajili ya mchezo dhidi ya Ethiopia.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Nigeria Samson Siasia amesema amekua akimfutilia kwa ukaribu mshambuliaji huyo huku akieleza kwamba atajisikia furaha sana endapo atatimiza ndoto zake za kumtumia katika mchezo huo.

Timu ya taifa ya Nigeria imepangwa katika kundi la pili lenye timu za Madagascar, Guinea pamoja na Ethiopia.

No comments:

Post a Comment