KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, March 1, 2011

GAME IPO PALE PALE HAKUNA MABADILIKLO.


Uongozi wa chama cha soka nchini Afrika kusini umekataa ombi la uongozi wa chama cha soka nchini Misri ambao ulitaka kusogezwa mbele kwa mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika kwa mwaka 2012 utakaozikutanisha nchi hizo.

Uongozi wa chama cha soka nchini Misri uliomba kusogezwa mbele kwa mchezo huo kwa ajili ya kutoa muda wa kutosha wa maandalizi ya kikosi chao ambacho kipo chini ya kocha Hassan Shehata.

Msemaji wa chama cha soka nchini Misri Amr Abu Elez amesema wameyapokea majibu hayo kwa uchungu mkubwa na ameeleza wazi kwamba hawana budi kucheza katika tarehe iliyopangwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF.

Amesema lengo lao kubwa kuomba tarehe ibadilishwe ni kutokana na kuwa na muda mchache wa kujiandaa ambapo muda mwingi wa kufanya hivyo ulimezwa na ghasia za kisiasa zilizojitikeza nchini Misri na kupelekea aliekua raisi wan chi hiyo Muhammad Hosni Sayyid Mubarak kujiuzulu.

Tarehe maalum iliyopangwa kwa ajili ya mchezo huo wa kundi la saba ni March 26 ambapo pia katika kundi hilo siku hiyo kutakakuwa na mchezo mwingine kati ya timu ya taifa ya Niger itaklua nyumbani dhidi ya Sierra Leone.

No comments:

Post a Comment