
Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Togo Emmanuel Sheyi Adebayor amesema angependelea kusalia mjini Madrid msimu ujao ili aweze kuitumikia klabu ya Real Madrid iliyomsajili kwa mkopo akitokea Man City ya nchini Uingereza.
Emmanuel Sheyi Adebayor aliesajiliwa kwa muda wa miezi sita amesema mazingira mazuri ya klabu ya Real Madrid yamekua akimvutia siku hadi siku hali ambayo inamsukuma kutamani kusajiliwa moja kwa moja.
Amesema amekua na mahusiano mazuri na kila mmoja klabuni hapo na hatua hiyo anaamini ndio inampa nafasi nzuri ya kucheza kwa kujiamini na pengine kufunga mabao pale inapotea nafasi anaopokua uwanjani.
Hata hivyo bado ameahidi kufanya makubwa ndani ya klabu hiyo ambayo anaamini yatawashawishi viongozi wa ngazi za juu ili waingine matamanio ya kufanya mipango ya kusajili moja kwa moja mwishoni mwa msimu huu.
Emmanuel Sheyi Adebayor alisajiliwa kwa mkopo mwezi Januri klabuni hapo baada ya kuwa na wakati mgumu kwenye kikosi cha klabu ya Manchester City ambacho kiliongezewa nguvu ya kusajiliwa kwa washambuliaji wawili ambao ni Super Mario Balotelli pamoja na Edwin Dzeko.
Tangu ajiunge na klabu ya Real Madrid mshambuliaji huyo tayari ameshacheza michezo 7 na amefunga mabao mawili.
No comments:
Post a Comment