
Uongozi wa klabu ya Tottenham Hoptspurs umetangaza kuwa kiungo wa kimataifa toka nchini Honduras pamoja na klabu hiyo Wilson Roberto Palacios Suazo atakua nje ya uwanja kwa kipindi cha majuma matatu yajayo.
Uongozi wa klabu hiyo umelazimika kutangaza taarifa hizo kufuatia Wilson Roberto Palacios Suazo kuumia goti akiwa mazoezini na tayari amefanyiwa vipimo ambavyo vimetoa msukumo kwa daktari wa klabu hiyo kushauri mchezaji kuyo kuwa nje ya uwanja kwa muda wa majuma matatu.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, alipata maumivu ya goti alipokua kwenye mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa hatua ya 16 bora wa michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya AC Milan uliochezwa siku ya jumatano ya juma hili huko jijini London.
Wilson Roberto Palacios Suazo ambae ameshaonekana uwanjani mara 30 msimu huu akiwa na kikosi cha Spurs, kwa mara ya mwisho alicheza mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Blackpool ambao walichomoza na ushidni wa mabao matatu kwa moja.
Kwa mantiki hiyo Wilson Roberto Palacios Suazo ataikosa michezo ya ligi kuu dhidi ya West Ham Utd pamoja na Wigan huku nafasi yake ikitarajiwa kuzibwa na Tom Huddlestone, Luka Modric, Jermaine Jenas ama kiungo wa kibrazil Sandro Ranieri GuimarĂ£es Cordeiro.
No comments:
Post a Comment