


Mahasimu wa soka mjini Manchester, Manchester City pamoja na Manchester United huenda wasiadhibiwe na chama cha soka nchini Uingereza kufuatia matukio yaliyojitokeza katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kombe la FA uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita katika uwanja wa Wembley.
Kamati ya nidhamu ya chama soka nchini Uingereza imekutana na kurejea mchezo huo kupitia picha za televisheni kwa lengo la kuthibitisha matukio hayo lakini imeelezwa kwamba huenda kamati hiyo ikashindwa kutoa kauli ya adhabu kutokana na matukio hayo kuonekana kawaida.
Moja ya matukio ambayo yalidhaniwa huenda yangeleta dhoruba kubwa na pengine kufungiwa na chama cha soka ni lile la mshambuliaji wa klabu ya Man City Super Mario Balotelli kuibusu nembo ya klabu hiyo mbele ya mashabiki wak labu ya Man Utd mara baada ya filimbi ya mwishi kupulizwa hatua ambayo ilipelekea mashabiki wa timu pinzani kumzomea.
Tukio lingine pia lilimuhusisha mshambuliaji huyo wa kimataifa toka nchini Italia dhidi ya beki wa klabu ya Man Utd Rio Ferdinand ambapo inadaiwa kwamba malumbano yaliyojitokeza kati ya wachezaji hao yalitokana na tambo ziliotolewa katika mtandao wa kijamii wa Twiter siku kadhaa kabla ya mchezo huo.
Inadaiwa kwamba Rio Ferdinand alichapisha maneno ya kumtahadharisha Super Mario Balotelli kwa kumueleza kwamba hatokua tayari kumuona analisakama lango lao kirahisi na kama itatokea hivyo atajihisi mkosefu katika maisha yake yote ya soka, hatua ambayo inatajwa kuwa chanzo cha wachezaji hao kulumbana kila walipokutana.
Hata hivyo hatua hiyo ya kupaniana kwa wachezaji hao wawili ilileta madhara makubwa pale Balotelli alipofikia wakati wa kukonyeza Rio Ferdinand ambae alikasirishwa na kitendo hicho na kupelekea mzozo uliotokea mbele ya meneja wa klabu na Man City Roberto Mancini ambae amekataa kuulizwa chochote juu ya hilo kwa kisingizo hakuona.
Katika mchezo huo wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la FA Man City walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri lililofungwa na kiungo wa kimataifa toka nchini Ivory Coast Yaya Toure katika dakika ya 52.
No comments:
Post a Comment