
Baada ya kupokea kisago cha mabao matano kwa sifuri kutoka kwa Stoke City katika mchezo wa jana wa hatua ya nusu fainali ya pili ya kombe la FA, meneja wa klabu ya Bolton Wanderers Owen Columba Coyle amesema hana budi kukubaliana na matokeo hayo.
Owen Columba Coyle ambae alitamba kuibuka kinara kabla ya mtanange huo kuunguruma amesema kiujumla kikosi chake hakikucheza vizuri na hali hiyo ilisabishwa na sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Wembley ambayo imekua ikilalamikiwa kila leo.
Amesema walipofika si haba na hakuna shabiki yoyote aliekua akiwapa nafasi kama wangeweza kucheza hatua ya nusu fainali ya kombe la FA msimu huu, hivyo hawana budi kujipongeza na kuhakikisha wanaendelea na utaratibu wa kufanya vyema kwenye michezo ya ligi ili waweze kumaliza katika nafasi nzuri.
Owen Columba Coyle pia akakisifia kikosi cha Stoke City kwa mchezo safi waliouonyesha na amewatakika kila na kheri katika mchezo wa hatua ya fainali ambapo watakutana na Man City May 14 katika uwanja wa Wembley.

Anthony Richard "Tony" Pulis meneja wa klabu ya Stoke City amesem ushindi mkubwa walioupata ni kiashirio kizuri kwa mashabiki wa soka ulimwenguni kote ambacho kinadhihirisha ubora wa kikosi chake ambacho kwa sasa kimedumu kwa misimu miwili katika michuano ya ligi kuu toka kilipofanikiwa kupanda daraja msimu wa mwaka 2008-09.
Amesema ushindi huo walioupata jana pia ni kazi nzuri inayofanywa kwa ushirikiano mkubwa kati ya benchi la ufundi, wachezaji, viongozi pamoja na mashabiki wa klabu hiyo yenye maskani yake makuu huko Britannia Stadium.
No comments:
Post a Comment