KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, April 19, 2011

Nuri Kâzım Şahin KUKOSA SEHEMU YA MSIMU.


Kiungo mchezeshaji wa mabingwa watarajiwa wa nchini Ujerumani Borussia Dortmund Nuri Kâzım Şahin hatojumuishwa katika kikosi cha klabu hiyo kwa kipindi cha msimu wa ligi kilichosalia.

Nuri Kâzım Şahin raia wa nchini Uturuki ameingia katika mazingira hayo baada ya kuumia goti la mguu wake wa kuli katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita pale Borussia Dortmund waliposhuka dimbani kuonyeshana umwamba na Freiburg waliokubali kisago cha bao moja kwa sifuri.

Daktari wa klabu ya Borussia Dortmund Markus Braun amesema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 aliumia vibaya katika maungio ya goti hivyo itamlazimu kupumzika kwa muda mrefu ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida.

Kwa mantiki hiyo sasa Borussia Dortmund watashuka dimbani mwishoni mwa juma hili bila ya kuwa na Nuri Kâzım Şahin anaewaniwa na klabu ya Real Madrid mwishoni mwa msimu huu na endapo vinara hao wa ligi ya Ujerumani wakishinda dhidi ya Borussia Mönchengladbach na Bayer Leverkusen wanaoshika nafasi ya pili wakapata matokeo ya sare ama kupoteza mchezo dhidi ya Hoffenheim watatawazwa kuwa mabingwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment