KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 16, 2011

Avram Grant ATOBOA SIRI YA KUSHUKA DARAJA.


Aliekua meneja wa klabu ya West Ham Utd Avram Grant amepasua ukweli wa kile kilichopelekea kikosi cha klabu hiyo kushuka daraja mara baada ya kushindwa kujihakikishai nafasi ya kubaki ligi kuu kwa ajili ya msimu ujao.

Avram Grant aliekua na matarajio makubwa ya kukinusuru kikosi cha klabu hiyo ya jijini London amesema utakata wa fedha unaoiandama West ham utd ulikuwa chanzo kikubwa cha yeye kushindwa kufikia mafanikio aliyojiwekea kabla ya kuanza kwa msimu.

Amesema ni masikitiko makuwa kwake kuona west ham utd inashuka daraja ikiwa mikononi mwake hali ambayo anaichukuliwa kama mkosi ambao unaendelea kumuandama hasa ikizingatiwa msimu uliopita Portsmouith ilishuka daraja ikiwa chini yake.

Mbali na kutoa sababu hiyo, Avram Grant pia akamuangushia lawama muamuzi aliechezesha pambano la jana kati ya West Ham utd dhidi ya Wigan Mike Dean kwa kusema kwamba alifanya maamuzi ya kutoa adhabu ndogo kwa wapinzani wao ambayo hakuyakubali hata kidogo.

Wakati huo huo meneja wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Redknapp amezungumzia masikitiko yake kufautia hatua ya kushuka kwa klabu ya West Ham Utd ambayo maskani yake makuu yapo jijini London sambamba na Spurs.


Amesema mazingira yaliyojitokeza hadi klabu hiyo inashuka daraja ni ya kusikitisha hususan katika mchezo wao wa jana ambapo kikosi cha The Hammers kilikua mbele kwa idadi ya mabao mawili kwa sifuri lakini mambo yaliwageukia na kutoa mwanya kwa Wigan kusawazisha na kuongeza bao la ushindi.

Redknapp bado akaendelea kukiri kwamba West Ham ni klabu nzuri na yenye utamaduni wa kipekee na anaamini muda si mrefu watarejea katika mbilinge mbilinge la ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Kama itakumbukwa vyema msimu uliopita West ham utd waliponea chupuchupu kushuka daraja baada ya kushika mkia kwa muda mrefu lakini ushindi wao dhidi ya Sunderland katika mchezo wa mwisho uliwaokoa na kuwabakisha katika ligi kuu.

No comments:

Post a Comment