KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 16, 2011

Sergio Busquets RUHUSA KUCHEZA FAINALI.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Hispania pamoja na klabu bingwa nchini humo Fc Barcelona Sergio Busquets atakua miongoni mwa wachezaji watakaocheza mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mbingwa barani Ulaya dhidi ya Man utd mwishoni mwa juma lijalo huko jijini londona kwenye uwanja wa Wembley.

Sergio Busquets alikua mashakani kuukosa mchezo huo kufuatia kesi ya ubaguzi wa rangi iliyokua ikimuandama huko UEFA baada ya uongozi wa klabu ay Real Madrid kuwasilisha malalamiko yao ambayo yalidai kwamba kiungo huyo alimtusi beki wa pembeni wa The Meringues Marcelo Vieira da Silva Júnior, wakati wa mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa FC Barcelona imesomeka kwamba kamati ya nidhamu ya UEFA iliyokua ikisikiliza kesi hiyo imetupilia mbali madai ya uongozi wa Real Madrid baada ya kushindwa kupatikana kwa ushahidi wa maneno yaliyotamkwa na kiungo huyo kwa lengo la kuashiria ubaguzi wa rangi.

Kufuati hatua hiyo FC Barcelona wamepewa baraka zote za kumtumia Sergio Busquets mwemye umri wa mika 22 katika mchezo wa hatua ya fainali, na kabla ya hatua hiyo ilielezwa kwamba endapo kiungo huyo angethibitika alitamka maneno ya ubagusi wa rangi huenda angefungiwa michezo mitano iliyo chini ya UEFA.

Sergio Busquets alituhumia kufanya kosa hilo kwa kumuita Marcelo Vieira da Silva Júnior, MONO MONO kwa lugha ya kispaniola, ambapo maneno hayo kwa lugha ya Kiswahili yanamaanisha NYANI NYANI.

No comments:

Post a Comment