KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, May 18, 2011

Gustavo Augusto "Gus" Poyet Domínguez SIENDI POPOTE.


Meneja wa klabu ya Brighton & Hove Albion ya nchini Uingereza Gustavo Augusto "Gus" Poyet Domínguez amekua mtu wa pili kutangaza kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha umeneja wa klabu ya West Ham Utd ambayo msimu ujao itashiriki ligi daraja la kwanza nchini humo.

Gus Poyet ametangaza hatua hiyo baada ya aliekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Steve Mclaren kufikia maamuzi kama hayo usiku wa kumkia jana ambapo alidai kwamba kwa sasa anahitaji muda wa kutuliza akili yake.

Gus Poyet amesema maamuzi aliyoyachukua yanatokana na yeye binafsi kutokua katika mipango ya kuomba nafasi hiyo zaidi ya kuhusishwa na taarifa zilizotolewa katika vyombo vya habari ambapo jina lake lilionekana likiwa sambamba na mameneja wengine.

Amesema jukumu kubwa alilonalo hivi sasa ni kuhakikisha kikosi chake cha klabu klabu ya Brighton & Hove Albion kinashiriki vyema ligi daraja la kwanza baada ya kukiwezesha kupanda kutoka ligi daraja la pili tena kwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Gus Poyet pia akaainisha wazi furaha yake ya kuendelea kuwepo ndani ya klabu ambayo inatarajia kuhamia katika uwanja mpya tena kwa kucheza ligi daraja la kwanza hivyo ni vigumu kwa upande wake kufanya maamuzi ya kuondoka huko Falmer Stadium.

No comments:

Post a Comment