KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, May 18, 2011

AC MILAN YAANZA KUJIZATITI KWA MSIMU UJAO.


Mabingwa wa soka nchini humo AC Milan wameendeleza azma yao ya kuhakikisha wanajiandaa vyema tayari kwa msimu ujao ambao utakuwa na upinzani mkubwa kufuatia ubingwa walioutwaa kabal ya kumalizika kwa msimu huu.

Sehemu ya azma ya mabingwa hao iliyokamilishwa mpaka sasa ni kuwasinisha mikataba mipya wachezaji waliokua wanamaliza mikatana yao mwishoni mwa msimu huu na tayari wameonekana kuwa muhimili mkubwa wa klabu hiyo ya San Siro.

Wachezaji hao waliosainishwa mikataba ni kiungo wa kimataifa toka nchini Uholanzi Mark van Bommel mwenye umri wa miaka 34 pamoja na beki wa kimataifa toka nchini Brazil Thiago Silva mwenye umri wa miaka 26.

Mark van Bommel amesainishwa mkataba mpya kufuatia ule aliousaini mwanzoni mwa mwaka huu alipojiunga na AC Milan akitokea Bayern Minich ya nchini Ujerumani kutarajia kufiki kikomo mwezi ujao, hivyo mkataba mpya utaendelea kumuweka huko San Siro hadi mwezi June mwaka 2012.Thiago Silva alijiunga na Ac Milan mwezi januari mwaka 2009 akitokea nchini kwao Braliz kwenye klabu ya Fluminese amesaini mkataba wa miaka mitano ambao utafikia kikomo mwaka w 2016.

Uongozi wa klabu ya AC Milan bado unaendelea na mchakato wa kuwapa mikataba mipya baadhi ya wachezaji wengine klabuni hapo ambapo inaelezwa kwamba awamu inayofuata itamuhusishwa kiungo wa kimataifa toka nchini uholanzi Clarence Seedorf, pamoja na viungo wa kitaliano Andrea Pirlo na Massimo Ambrosini.

No comments:

Post a Comment