KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, May 18, 2011

KAKA ATHIBITISHA UWEPO WAKE MJINI MADRID MSIMU UJAO.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Brazil Ricardo Izecson dos Santos Leite Kaka amekanusha vikali taarifa za kuwa mbioni kuhamia jijini London ambazo ziliripotiwa siku mbili zilizopita huko nchini Uingereza.

Kaka amekanusha taarifa hizo huku akidai kwamba bado anaipenda Real Madruid na yupo mjini Madrid kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo ambayo ilimsajili akitokea nchini Italia kwa mabingwa wa soka nchini humo AC Milan na hiyo ilikua mwaka 2009.

Amesema suala la mama yake mzazi kuhamia jijini London halihusiani na maisha yake ya baadae, tena amewataka mashabiki wake pamoja na wale wa Real Madrdi kutambua kwamba ataendelea kuwepo huko Estadio Stantiago Bernabeu.

Hata hivtyo amekiri kwamba mama yake mzazi ambae anafanya shughuli za kuhubiri neno la mungu ni kweli anakwenda kuishi jijini London mwaka ujao na sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kufuatia shughuli zake za kikanisa.

Kaka kwa muda mrefu amekua akihusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na klabu ya Chelsea kwa kisingizio cha kufanya kazi na meneja wake wa zamani Carlo Ancelotti.

No comments:

Post a Comment