KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, May 28, 2011

NI KOSA KUBWA ENDAPO REDKNAPP ATAPEWA RUHUSA NA YA KUONDOKA - BALE.
Winga wa kimataifa toka nchini Wales pamoja na klabu ya Tottenham Hostpurs Gareth Bale amemtahadharisha mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy kufuatia suala la meneja Harry Redknapp kuhusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na klabu ya Chelsea.


Gareth Bale ametoa tahadhari hiyo kwa Daniel Levy kwa kusema kwamba endapo meneja huyo ataachiwa na kuondoka klabuni hapo mafanikio yaliyoaanza kuonekana yataingia gizani na huenda Spurs ikapoteza muelekeo wa ushindani.

Amesema kuna umuhimu mkubwa wa meneja huyo wa kingereza kubaki klabuni hapo hasa ikizingatiwa amekua akihusia suala la mshikamano kwa wachezaji pamoja na benchi zima la ufundi hali ambayo imekua ikichangia kupatikamna kwa matokeo mazuri.


Winga huyo mwenye umri wa miaka 21 ameongeza kwamba kuajiriwa kazi kwa meneja huyo mwaka 2008 mara baada ya kutimuliwa kwa meneja wa kispaniola Juande Ramos mabadiliko mengi yamejitokeza hivyo hakuna namna ya kuanza kutoa nafasi kwa Redknapp kuondoka kama inavyodhaniwa na wengi.

Hata hivyo tayari Harry Redknapp ameshakanusha taarifa za kuwa tayari kujiunga na klabu hiyo ya magharibi mwa jijini London ambayo mwishoni mwa juma lililopita ilimtimua kazi Carlo Michelangelo Ancelotti.

No comments:

Post a Comment