KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, May 28, 2011

NI PATASHIKA NGUO KUCHANIKA KATIKA VITA YA KUINUNUA ARSENAL.


Mfanyabiashara wa kimarekania anaemiliki sehemu kubwa ya hisa za klabu ya Arsenal Stan Kroenke amewashiwa taa ya kijani katika utaratibu wake wa kutaka kuinunua klabu hiyo kufuatia uongozi wa kamati ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza kuthibitisha utambuzi wa umiliki wake.

Taarifa iliyotolewa na kamati hiyo iliyo chini ya chama cha soka nchini Uingereza imeeleza kwamba Kroenke ambae kwa sasa anamiliki asilimia 66.06 natambulika kama mtu wenye kauli ya mwisho hatua ambayo imethibitishwa pia ya uongozi wa klabu ya Arsenal ambao upo chini ya mwenyekiti Danny Frizman.

Hatua hiyo inamuwezesha mfanyabiashara huyo kutoka nchini marekani kuendelea na mikakati ya kuhakikisha anambebeleza mwana hisa mwenzake Alisher Usmanov anaemiliki asilimia 27.37 ili aweze kununua hisa zake.

Stan Kroenke alipata nafasi ya kuongeza asilimia ya hisa zake baada ya kununua hisa za Lady Nina Bracewell-Smith pamoja na Danny Fiszman ambae kwa sasa ni marehemu.


Wakati huo huo kampuni ya Red & White vehicle inayomilikiwa na Alisher Usmanov imetoa taarifa zinazodai kwamba bilionea huyo wa kirusi ameongeza hisa zake kutoka asilimia 27 hadi asilimia 28.

Hatua hiyo ya kuongeza hisa kwa Alisher Usmanov imedhihirisha wazi kwamba Stan Kroenke bado ana wakati mgumu wa kuendelea kumbembeleza bilionea huyo.

Hata hivyo tayari Stan Kroenke ameshatangaza kununua kila hisa ya bilionea huyo kwa kiasi cha paund 11,750 lakini ombi hilo liliwekwa kapuni na Alisher Usmanov huku akisema hayupo tayari kuuza hisa zake.

No comments:

Post a Comment