KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, May 18, 2011

Roberto Mancini AWAONDOA HOFU MASHABIKI WA MAN CITY.


Meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini amewaondoa hofu mashabiki wa klabu hiyo kwa kusema mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Carlos Tevez amemsisitizia jambo la kubaki klabuni hapo kama mkataba wake unavyoelekeza.

Roberto Mancini amewaondoa hofu mashabiki wa klabu ya Man City baada ya kujibu swali aliloulizwa na waandishi wa habari mara baada ya mchezo wa ligi uliochezwa usiku wa kumkia hii leo huko City Of Manchester ambapo wenyeji walifanikiwa kupata ushindi wa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Stoke City.

Roberto Mancini amesema mara baada ya kikosi chake kufanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la FA mwishoni mwa juma lililopita, Carlos Tevez alimthibitishia kwamba yu tayari kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambayo amedai imeonyesha muelekeo wa kupatikana kwa mafanikio zaidi ya waliyoyapata msimu huu.

Amesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekua mstari wa mbele kuhakikisha kila jambo linakwenda vizuri kikosini hivyo anaamini kubaki kwake kutasaidia hatua ya kuongeza chachu ya yale waliyoyaopanga kwa ajili ya msimu ujao.Wakati huo huo meneja wa klabu ya Stoke City Tonny Pulis amekiri kikosi cha Man city kimekomaa kimchezo pamoja na upinzani kufuatia kuonyesha soka safi toka alipoanza kukutana nacho katika mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la FA mpaka katika mchezo wa jana wa ligi.

Amesema kikosi cha klabu hiyo kimebadilika mbali na msimu uliopita hivyo anaamini ushiriki wake katika michuano ya kimatafa msimu ujao utaleta changamito kwa vilabu vyenye uzoefu na michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment