KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, May 18, 2011

IMA HUKU AMA KULE KWA Torsten Frings.


Uongozi wa klabu ya Werder Bremen, umempa masharti kiungo wa klabu hiyo Torsten Frings ambae mkataba wake unatarajia kufikia kikomo mwishini mwa msimu huu.

Masharti aliyopewa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34, ni kuwa tayari kuondoka klabuni hapo akiwa kama mchezaji huru ama kubaki ili awezeshwe kujiendeleza katika masomo ya ukocha kwa ajili ya kuendeleza mazuri ndani ya Werder Bremen siku za usoni.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Klaus Allofs amesema Torsten Frings amepewa masharti hayo baada ya uongozi wa Weder Bremen kukaa chini na meneja wao Thomas Schaaf ambae alishauri utaratibu huo ufanywe kutokana na kiungo huyo kutokuwemo kwenye mipango yake ya hivi sasa.

Klaus Allofs amesema uongozi umefikiria hivyo kwa lengo la kutaka kuendelea kuwa na Torsten Frings klabuni hapo kwa siku za usoni na kuheshimu mchango wake mkubwa alioutoa toka alipoelekea huko Weserstadion mwaka 2005.

Hata hivyo Torsten Frings ameonyesha kuyakataa masharti hayo kwa kusema kwamba bado anahitaji kucheza soka na kumaliza akiwa katika mazingira mazuri hivyo kama itashindikana atasaka klabu nyingine kwa jili ya kuendeleza ndoto yake.

No comments:

Post a Comment