KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, May 21, 2011

UFARANSA WATANGAZA VIWANJA VYA 2016.


Wakati nchi za Poland pamoja na Ukraine zikiendelea na maandalizi ya fainali za mataifa ya barani Ulaya zitakazoanza kutimua vumbi lake June 8 – July Mosi mwaka ujao, wenyeji wa fainali hizo kwa mwaka 2016 Ufaransa hii leo wametaja viwanja vitakavyotumika.

Ufaransa waliofanikiwa kushinda harakati za kuwa mwenyeji wa fainali za mataifa ya bara la Ulaya kwa mwaka 2016 baada ya kuzishinda nchi za Italia pamoja na Uturuki wametangaza viwanja tisa vilivyopo katika miji minane tofauti.

Taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa shirikisho la soka la nchi hiyo imefafanua kwamba viwanja viwili kati ya hivyo vipo mjini Paris ambvyo ni Stade de France pamoja na Parc des Princes huku vingine vikiwa katika mji wa Marseille ambacho ni Stade Velodrome, mji wa Nancy ni Stade Marcel Picot, mji wa Lille ni Grand Stade Lille Métropole, mji wa Lyon ni Stade des Lumières, , mji wa Lens ni Stade Felix-Bollaert, pamoja na mji wa Nice ni Grand Stade Nice huku mji wa Bordeaux uwanja wake bado unatengenezwa kwa hivi sasa.

Katika fainali za mataifa ya barani ulaya kwa mwaka huo historia mpya itaandikwa kufuatia timu shiriki kutarajia kuongezea kutoka 16 hadi 24.

No comments:

Post a Comment