KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 14, 2011

Alexis Sanchez AWEKWA SOKONI KWA MIPESA KIBAO.


Homa ya usajili wa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Udinese Alexis Sanchez imeendelea kupanda huku vilabu kadhaa vya barani Ulaya vikiendelea kupigana vikumbo katika harakati za kuiwani saini ya mchezaji huyo.

Homa ya usajili wa Sanchez imeendelea kuwa juu kufuatia dau lake kutangazwa na mmiliki wa klabu ya Udinese Gianpaolo Pozzo ambapo amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kiungo huyo atapewa ruhusa ya kujiunga na klabu itakayomsajili kwa ada ya uhamisho wa euro million 35 (£31million).

Hata hivyo mmiliki huyo amesema mpaka sasa hakuna klabu hata moja iliyowasilisha ofa ya kutaka kumsajili Sanchez huko Stadio Friuli, zaidi ya maneno kuzungumzwa kupitia vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa malelezo yanayotolewa na vyombo mbali mbali vya habari barani Ulaya, kiungo huyo wa kimataifa kutoka nchini Chile anawindwa vikali na klabu ya Manchester City, Barcelona pamoja na Inter Milan.

No comments:

Post a Comment