
Klabu tano za barani Ulaya zimeripotiwa kukubali ofa ya kumsajili mshambukliaji chipukizi wa klabu ya Santos ya nchini Brazil Neymar da Silva Santos Júnior ambae pia huichezea timu ya taifa ya nchi hiyo.
Akizungumza kwa asharti la kutozitaja klabu hizo raisi wa klabu ya Santos Luis Alvaro de Oliveira Ribeiro amesema wamekua na mawasiliano mazuri na viongozi wa klabu hizo za barani Ulaya na kila mmoja amekua akihitaji kupewa muda wa kuzungumza na mshambuliaji huyo kwa ajili ya kukubaliana masuala binafsi.
Luis Alvaro de Oliveira Ribeiro amesema sharti waliloweka baada ya kuona klabu hizo zina mipango ya kutaka kumsajili Neymar da Silva Santos Júnior ni ada ya uhamisho wake ambayo ni paund million 40.
Hata hivyo Luis Alvaro de Oliveira Ribeiro amedai kwamba wao kama viongozi wa klabu ya Santos hawakuwa tayari kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19, lakini kutokana na mazingira yaliyopo wamelazimika kufanya hivyo, ambapo pia mkataba wake unaruhusu kukamilishwa kwa suala la kusajiliwa na klabu nyingine.
Pamoja na klabu hizo kutokutajwa na Luis Alvaro de Oliveira Ribeiro, imefahamika kwamba klabu zilizokua zikipigana vikumbo kwa maneno kwa ajili ya kumsajili Neymar da Silva Santos Júnior ndizo zimekubali kumsajili kwa ada ya uhamisho iliyowekwa wazi na viongozi wa klabu ya santos.
Klabu hizo ni Real Madrid na Barcelona za nchini Hispania, Chelsea pamoja na Manchester City za nchini Uingereza na klabu Anzhi Makhachkala ya nchini urusi.
Mpaka sasa Neymar da Silva Santos Júnior ameshafanikiwa kuichezea klabu ya Santos michezo 63 na kupachika mabao 27, na bao la kwanza akiwa na klabu hiyo iliyomkuza alilifunga December 2009 katika mchezo wa ligi dhidi ya Cruzeiro.
No comments:
Post a Comment