KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 28, 2011

Sílvio Manuel Ferreira AIHAMA FC BRAGA.


Pengo lililoachwa na beki wa Jamuhuri ya Czech Tomáš Ujfaluši huko Estadio Vicente Calderón, limefanikiwa kuzibwa na viongozi wa klabu ya Atletico Madrid baada ya kufanikisha utaratibu wa kumsajili beki kutoka Fc Braga ya nchini Ureno Sílvio Manuel Ferreira.

Sílvio Manuel Ferreira amejiunga na klabu hiyo ya mjini Madrid ikiwa ni baada ya majuma kadhaa kuweka hadharani mipango yake ya kutaka kuihama Fc Braga ambayo ilishindwa kutwaa ubingwa wa ligi ya barani Ulaya mbele ya Fc porto mwishoni mwa mwezi uliopita huko nchini Poland.

Usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 23, unaaminiwa utaleta changamoto mpya katika safu ya ulinzi klabuni hapo baada ya kuuzwa kwa Tomáš Ujfaluši ambae amejiunga na klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki.

Sílvio Manuel Ferreira amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano ambao utamuweka Estadio Vicente Calderón hadi June 27 mwaka 2016, na hii leo alitarajiwa kutambulishwa kwa waandishi wa habari.

Wakati huo huo mlinda mlango wa klabu ya Liverpool José Manuel "Pepe" Reina Páez amesema hana mpango wa kutaka kurejea nyumbani kwao Hispania kwa ajili ya kujiunga na klabu ya Atletico Madrid.

Jose Pepe Reina ametangaza msimamo huo kufuatia vyombo vya habari nchini Hispania kuripoti kwamba kipa huyo mwenye umri wa miaka 28, yupo kwenye mipango ya kusajiliwa na klabu hiyo ya mjini Madrid kama sehemu ya kuziba nafasi inayoaachwa wazi na Davd De Gea alie mbioni kujiunga na mabingwa nchini Uingereza Man utd.

No comments:

Post a Comment