KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, July 15, 2011

Alexis Sanchez KUTUA FC BARCELONA !!


Mabingwa wa soka nchini humo pamoja na barani Ulaya kwa ujumla FC Barcelona wamekubali kumsajili mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Chile pamoja na klabu ya Udinese ya nchini Italia Alexis Sanchez.

Fc Barcelona wamekubali kumsajili mshambuliaji huyo kwa ada ya uhamisho wa paund million 27 ambayo imeafikiwa baada ya kukamilika kwa mazungumzo ya pende zote mbili ambayo yamedumu kwa siku kadhaa zilizopita.

Pesa hizo ambazo zitalipwa kama ada ya uhamisho wa Sanchez, zitawasilishwa Stadio Friuli mara baada ya mchezaji huyo kufanyiwa vipimo na kuthibitika anakidhi viwango vya afya vinavyotakikana huko Camp Nou.

Hata hivyo kwa sasa Alexis Sanches, bado yupo nchini Aregntina akiwa na timu ya taifa lake la Chile ambalo bado linaendelea kumsaka mwali wa fainali za mataifa ya kusini mwa bara la Amerika *Copa America*.

Kukamilika kwa mazungumzo ya kuuzwa kwa Sanchez kunamaliza zogo la uhamisho wa mchezaji huyo lililodumu kwa muda mrefu ambapo klabu kadhaa zilihusishwa kutoka barani Ulaya ambapo miongoni mwa klabu hizo ilikuwepo Man utd, Man city, Inter Milan, Real Madrid pamoja na Juventus.

No comments:

Post a Comment