KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 19, 2011

MAN CITY NA MIPANGO YA USAJILI.


Siku moja baada ya kuwataka mashabiki wa Man city kuwa watulivu katika mipango ya kuziba nafasi itakayoachwa wazi na Carlos Tevez alie mbioni kurejea nchini Brazil, meneja wa klabu hiyo Roberto Mancini amesema anajiandaa kutuma ofa ya kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Argentina Sergio Aguero.

Roberto Mancini ametangaza mpango huo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya kikosi chake dhidi ya kikosi cha Vancouver Whitecaps ambao ulimalizika kwa Man City kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Amesema hana budi kufanya mikakati ya kumsajili mchezaji huyo ambae anahusishwa na taarifa za kuihama Atletico Madrid na anaamini endapo atafanya hivyo kutakuwa na kila sababu za kuendelea kufanya vyema msimu ujao.

Nae kiungo wa Man City Gareth Barry ameunga mkono mpango huo wa kutaka kusajiliwa kwa Sergio Aguero ambae amemwagia sifa kedekede ambazo zinambeba na kumvisha jukumu la Carlos Tevez.

Amesema mshambuliaji huyo ana vigezo vya kutosha na anaamini atakisaidia kwa kiasi kikubwa kikosi cha Man city ambacho msimu ujao kimepania kufanya makubwa zaidi ya yale yaliyofanywa msimu wa mwaka 2010-11.

Gareth Barry pia akagusia suala la kutarajia kuondoka kwa Carlos Tevez ambapo amesema linastahili kuheshimiwa kama msimamo wake.

No comments:

Post a Comment