KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 19, 2011

DOGO WA CHELSEA KWENDA KWA MKOPO HISPANIA.

Kipa kutoka nchini Ubelgiji Thibaut Courtois, alie mbioni kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Chelsea, huenda akapelekwa kwa mkopo Atletico Madrid wanaomsaka mrithi wa David de Gea aliesajiliwa na mabingwa wa soka nchini Uingereza Man Utd.

Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 19, anafikiriwa kupelekwa nchini Hispania kufuatia hitaji lake la kutaka kucheza kila juma, ambalo kwa sasa halitowezekana akiwa ndani ya kikosi cha Chelsea ambacho kinamtegemea sana kipa kutoka jamuhuri ya Czech Peter Cech.

Taarifa hizo za kupelekwa kwa mkopo mjini Madrid mara baada ya usajili wake kukamilika huko Stamford Bridge, zimepokelewa vyema na kipa huyo ambapo amesema bado ni faida kwake kutokana na kutaka kutimiza lengo la kucheza kila juma.

Amesema anatambua bado nafasi yake ndani ya kikosi cha Chelsea ipo na katu haitopotea, hasa ikizingatiwa ana umri mdogo ambao unampa fursa wa kukiendeleza kipaji chake popote pale ulimwenguni.

Thibaut Courtois, pia akathibitisha furaha aliyonayo ya kutarajia kucheza sanjari na Frank Lampard, John Terry pamoja na Didier Drogba ambao amesema kwa kipindi kirefu alikua akiwaona kupitia televisheni.

Wakati huo huo kiungo na nahodha msaidizi wa kikosi cha chelsea Frank Lampard amesema msimu ujao watakua imara zaidi ya msimu uliopita na hawatokua na sababu za kushindwa kurejesha ubingwa nyumbani baada ya kuupoteza mikononi mwa Man Utd.

Amesema mipango ya meneja wao mpya Andre villas Boas ukiwepo mpango wa usajili wa wachezaji unawapa imani hiyo ambayo pia inatoa changamoto kwa mashabiki wa The Blues.

No comments:

Post a Comment