
Mabingwa wa kombe la FA Manchester City wameendelea kujizatiti katika usajili, baada ya kufanikiwa kumnasa beki kutoka nchini Montenegro Stefan Savic kwa ada ya uhamisho wa paund million 10 akitokea kwenye klabu ya Partizan Belgrade ya nchini Serbia.
Man City wamekamilisha dili hilo baada ya Stefan Savic, kufanyiwa vipimo vya afya jana jioni ikiwa ni sehemu ya uhamisho wake katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini Uingreza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anakua mchezaji wa pili kusajiliwa huko City Of Manchester ikiwa ni baada ya siku mbili kupita ambazo zilishuhudia beki wa pembeni wa kifaransa Gael Clichy akikamilisha usajili wake akitokea Arsenal.
Stefan Savic anaecheza nafasi ya beki wa kati kati siku za awali za kipindi hiki cha usajili alikuwa akihusishwa na taarifa za kutakiwa na klabu ya Arsenal ambayo ilikua tayari kutoa kiasi cha paund million mbili kabla ya dau lake kupanda na kufikia paund million 10 baada ya Man city kutangaza nia kama hiyo.
Katika hatua nyingine matajiri hao wa mjini Manchester, wametangaza kuwa tayari kumsajili kiungo wa klabu ya Arsenal Samir Nasri ambae yu mbioni kuihama klabu hiyo ya jijini London.
Man City wametangaza kuwa tayari kufanya hivyo huku wakianika wazi mipango yao ya kumlipa mshahara mchezaji huyo wa paund 150,000 kwa juma sambamba na kutoa kiasi cha paund million 20 kama ada ya uhamisho wake kutoka kaskazini mwa jiji la London.
Kama itakumbukwa vyema Samir Nasri tayari ameshatangaza nia ya kutaka kujiunga na klabu yenye kiu ya kusaka majati msimu ujao, baada ya kushindwa kufanya hivyo akiwa na Arsenal kwa muda wa misimu mitatu mfululizo.
No comments:
Post a Comment