
Mabingwa wa CONCACAF Mexico wameanza vibaya kampeni za kusaka ubingwa wa fainali za mataifa ya bara la Amerika ya kusini *COPA AMERICA* baada ya kukubali kichapo cha mabao mawili kwa moja kilichotolewa na timu ya taifa ya Chile.
Mabao yaliyofungwa na Esteban Paredes pamoja na Arturo Vidal yalizima ndoto za Mexico kuanza kwa makeke kwenye fainali hizo huku wakichagizwa na ubingwa wa CONCACAF walioupata majuma mawili yaliyopita baada ya kuishinda timu ya taifa ya Marekani.
Hata hivyo mchezo huo wa kundi la tatu, ulitawaliwa na upinzani mkubwa kutokana na kila upande kuonyesha soka safi wakati wote 19 wa mchezo huku kinda Nestor Araujo mwenye umri wa miaka akiifungia bao la kuongoza kwa upande wa Mexico.
Mchezo mwingine wa kundi hilo ulikua kati ya timu ya taifa ya Uruguay dhidi ya timu ya taifa ya Peru, ambapo matokeo ni kwamba timu hizo zimetoshana nguvu kwa kufungana bao moja kwa moja.
Hii leo fainali hizo zinaendelea tena kwa kushuhudia wenyeji Argentina wakitupa karata yao ya pili kwa kucheza na timu ya taifa ya Colombia.
Katika mchezo wa kwanza timu ya taifa ya Argentina al-manusura ipokee kichapo kutoka kwa Bolivia lakini shukrani za kipekee zimuendeee mshambuliaji wa Atletico Madrid Sergia Aguero katika dakika ya 47 kipindi cha pili.
Colombia wao wataingia uwanjani hii leo huku wakichagizwa na ushindi wa bao moja kwa sifuri walioupata katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Costa Rica.
Mchezo mwingine wa kundi hilo la kwanza utakua kati ya timu ya taifa ya Bolivia dhidi ya Costa Rica.
No comments:
Post a Comment