KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 15, 2011

Fernando Torres AWAAHIDI MAKUBWA MASHABIKI.

Mshambuliaji kutoka nchini Hispania Fernando Torres amewataka mashabiki wa Chelsea kuwa watulivu na kuonyesha ustahamilivu dhidi yake katika msimu huu wa ligi kuu ya soka nchini UIngereza ulioanza mwishoni mwa juma lililopita.

Torres ametoa rai hiyo kwa mashabiki wa The Blues huku akiwaahidi kufanya makubwa zaidi ya yale aliyo yaonyesha akiwa na klabu ya zamani Liverpool ambapo huko kila mmoja alimpenda kwa shughuli ya upachikaji mabao.

Amesema kinachotakiwa kwa sasa kila shabiki wa Chelsea asahau yaliyopita na kutazama mbele, huku akimini kikosi chao kipo kwa ajili ya kuwapa raha msimu huu baada ya ubingwa kuwaponyoka msimu uliopita na kuelekea Old Trafford.

Fernando Torres jana alijumuishwa katika kikosi cha Chelsea kilicholazimishwa sare bila kufungana dhidi ya Stoke City, ambapo alionyesha uwezo mkubwa lakini alikutana na changamnoto kadha wa kadha kutoka kwenye safu ya ulinzi ya timu pinzani.

Wakati huo meneja wa Chelsea Adre Villas Boas ametanabaisha kwamba wachezaji wake walionyesha uwezo na kujituma ipasavyo lakini umahiri wa safu ya ulinzi ya Stoke city ulikua kikwako kufikia malengo ya ushindi na mwisho wa siku walijikuta wakipata matokeo ya sare.

Adre Villas Boas pia amekataa kuzungumza lolote juu ya maamuzi mabovu ya kunyimwa penati mbili ambazo mashabiki wengi wa Chelsea wamekua wakilalamika juu ya suala hilo kwa kusema muamuzi wa mchezo wa jana wamechangia kukosa kwao ushindi.

Nae meneja wa Stoke City Tonny Pulis amesema hana budi kuwashukuru wachezaji wake kwa kazi nzuri waliyoifanya hasa ikizingatiwa wamecheza na kikosi chenye uwezo mkubwa katika ligi ya nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment