KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 20, 2011

Alberto Gilardino NJE WIKI SITA.

Mshambuliaji kutoka nchini humo pamoja na klabu ya Fiorentina Alberto Gilardino atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa majuma sita yajayo kufuatia maumivu ya goti la kushoto yanayomkabili.

Mshambuliaji huyo alipatwa na maumivu hayo makali mwishoni juma lililopita baada ya kugongana na kipa wa klabu ya Udinese Samir Handanovic akiwa katika purukushani za kutaka kufunga.

Hata hivyo uongozi wa klabu ya Fiorentina umedai kwamba huenda Alberto Gilardino akawahi kurejea uwanjani kutokana na matibabu atakayopatiwa na daktari mkuu wa klabu hiyo ambae pia amewathibitishia kuwepo kwa uwezekano huo.

Katika mchezo huo wa ligi ya Sirie A, Fiorentina walikubali kisago cha mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Udanise.

No comments:

Post a Comment