KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 20, 2011

MANCINI KUMSAJILI DANIELE DE ROSI MWEZI JANUARI?

Meneja Man city Roberto Mancini bado ana dhamira ya kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Italia na klabu ya AS Roma Daniele De Rossi ambae tayari ada yake ya uhamisho imeshatangazwa hadharani kuwa ni paund million 8.

Roberto Mancini ameendelea kuonyesha dhamira hiyo kutokana na kukiri kwamba kikosi chake kinahitaji kuongezewa nguvu kutokana na muonekano wa kilivyo sasa hali ambvayo anaamini ilipelekea matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Fulham mwishoni mwa juma lililopita.

Katika kipindi cha usajili kilichofikia kikomo usiku wa kuamkia Septemba mosi, meneja huyo alitamani kumsajili Daniele De Rossi lakini sheria za ligi kuu ya soka nchini Uingereza za kutaka wachezaji watano kutoka nje ya nchi hiyo zilimbana na mwishowe alilazimika kumsajili Owen Hargreaves aliekua mchezaji huru akitokea Man utd.

Hata hivyo tayari baadhi ya vyombo vya habari nchini italia vimeripoti kwamba Daniele De Rossi huenda akajiunga na Man city mwezi Januari baada ya kugoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo huku mkataba wake wa sasa ukitarajia kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Wakati huo huo uongozi wa klabu ya Manchester City umetangaza mpango wa kujenga viwanja vya mazoezi ambavyo vitawafanya wafanane na mabingwa wa soka nchini Hispania pamoija na barani Ulaya kwa ujumla Fc Barcelona.

Man City wametangaza mpango huo huku serikali ya mjini Manchester ikiwa tayari imeshawapa nafasi ya kuendelea na mpango huo ambao utawapa nafasi ya kuingia katika utawala tofauti katika medani ya soka.

Lengo kubwa la uongozi wa klabu hiyo ni kutaka kukuza na kuwaendeleza vijana kama ilivyo kwa Fc Barcelona ambao wanaendelea kufanya hivyo, na kwa sasa matunda yake yanaonekana kupitia kwa Lionel Messi, Cesc Fabregas, Andres Iniesta pamoja na wachezaji wengine ambao walikuzwa katika kituo cha La Masia.

No comments:

Post a Comment