KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 21, 2011

Andre Villas-Boas AKIRI KUAGIZWA NA BOSI WAKE.

Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich amemtaka meneja wake Andre Villas-Boas kuitumia michuano ya kombe la ligi kama sehemu ya kuwaendeleza vijana wa klabu hiyo.

Akithibitisha agizo hilo alipokutana na waandishi wa habari meneja huyo mwenye umri wa miaka 33 amesema Roman Abramovich amesema atafurahishwa mno endapo ataiona klabu yake inakuza na kuwaendelea vijana watakaokua watetezi wazuri wa The Blues siku za usoni.

Amesema agizo hilo limekuja, kufuatia mafanikio makubwa yaliyoonekana katika klabu jirani ya Arsenal chini ya utawala wa Arsene Wenger ambayo kwa kipindi kirefu imekua ikiwatumia wachezaji wenye umri mdogo katika michuano ya komba la ligi.

Andre Villas-Boas amesema kwa mantiki hiyo katika mchezo wa hii leo dhidi ya Fulahm anatarajia kuwatumia wachezaji kama Romelu Lukaku na Josh (Macksharan )McEachran wenye umri wa miaka 18, Oriol Romeu mwenye umri wa miaka 19, Ryan Bertrand mwenye umri wa miaka 22 pamoja na Nathaniel Chalobah mwenye umri wa miaka 16.

Amesema siku za nyuma Chelsea ilikua ikutumia mfumo huo kwa kuwachezesha wachezaji wenye umri mdogo katika michuano ya kombe la ligi, lakini ujio wa Jose Mourinho ulifuta mfumo huo na kuanza kuwatumia wachezaji wenye umri mkubwa tena wanaocheza katika kikosi cha kwanza kutokana na mahitaji ya klabu yalikua yakilenga kutwaa ubingwa wa kwanza ambao ulikua wa Curling Cup.

Amesema melengo yao kwa sasa ni kutwaa vikombe vyote vya michuano wanayoshiriki hivyo anahitaji kila mchezaji kushirikishwa katika mtiririko huo.

Michezo mingine ya hatua ya tatu ya kombe la ligi itakayochezwa usiku huu ni pamoja na:


Amex Stadium,
Brighton and Hove Albion v Liverpool

Cardiff City Stadium,
Cardiff City v Leicester City

Etihad Stadium,
Manchester City v Birmingham City

St. Mary's Stadium,
Southampton v Preston North End

Goodison Park,
Everton v West Bromwich Albion


No comments:

Post a Comment