KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 21, 2011

MICHAEL OWEN MOTO MKUBWA !!!.

Mabao mawili kati ya matatu yaliyofungwa na mshambuliaji kutoka nchini Ungereza Michael Owen dhidi ya Leeds Utd huko Elland Road, yamemlazimu meneja wa Man utd Sir Alex Ferguson kumpa tano mshambuliaji huyo kwa kazi kubwa aliyoifanya.

Sir Alex Ferguson amesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 bado ana uwezo mkubwa anapokua uwanjani mbali na wengi walivyokua wakimfikiria kabla ya mpambano wa jana wa kuwania kombe la ligi.

Amesema Michael Owen kwa sasa hana tofauti na mshambuliaji wake kutoka nchini Mexico Javier Hernández Balcázar Chicharito, Wayne Rooney pamoja na Dimitar Ivanov Berbatov ambae anatokea nchini Bulgaria.

Bao la tatu katika mchezo huo lilifungwa na mkongwe Ryan Giggs katika dakika ya 43 huku bao la kwanza la pili yakifungwa katika dakika ya 15 na 32.


Matokeo ya michezo mingine ya hatua ya tatu ya michuano hiyo ya kombe la ligi ni pamoja na:

Recreation Ground.
Aldershot Town 2 - 1 Rochdale

Villa Park.
Aston Villa 0 - 2 Bolton Wanderers

Turf Moor.
Burnley 2 - 1 Milton Keynes Dons FC

City Ground.
Nottingham Forest 3 - 4 Newcastle United

Britannia Stadium.
Stoke City 0 – 0 (7-6) Tottenham Hotspur

Molineux.
Wolverhampton Wanderers 5 - 0 Millwall

Ewood Park.
Blackburn Rovers 3 - 2 Leyton Orient

Crystal Palace 2 - 1 Middlesbrough
Selhurst Park.

No comments:

Post a Comment