KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 19, 2011

ASHLEY COLE HAKUSTAHILI KADI YA NJANO.

Uongozi wa chama cha soka nchini Uingereza umesema beki wa pembeni wa klabu ya Chelsea Ashley Cole hatochukuliwa hatua za kisheria kufuatia rafu aliyomchezea mshambuliaji wa Man utd Javier Hernández Balcázar Chicharito katika mchezo wa jana huko Old Trafford.

Uongozi wa chama cha soka nchini humo umelazimika kulitoa ufafanuzi suala hilo kufuatia malalamiko yaliyotolewa na meneja wa Man utd ambae alidai Ashley Cole alistahili kuonyeshwa kadi nyekudu kufuatia kosa alilolifanya na si adhabu ya kadi ya njano aliyoonyeshwa na muamuzi Phil Dowd.

Ufafanuzi huo umetolewa kwa kigezo cha sheria za shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA ambazo zinaeleza kwamba mchezaji hawezi kuchukulia hatua zaidi ya adhabu aliyopewa na muamuzi wa mchezo husika hivyo bado beki huyo anaendelea kuhesabika kuwa miongoni mwa wachezaji walioadhibiwa kwa kadi ya njano.

Hata hivyo sheria hiyo inaelezea kwa upande wa pili ambapo mchezaji ataadhibiwa na shirikisho ama chama cha soka cha nchi husika endapo atafanya kosa ambalo halikuonekana na muamuzi wa mchezo wa ligi ama mashindano makubwa duniani lakini likaonekana kwa njia tofauti.

Wakati huo huo meneja wa Chelsea Andre Villas-Boas amesisistiza kwamba kupoteza mchezo wa jana kwa kufungwa mabao matatu kwa moja hakuwezi kuwapotezea nafasi ya kufikia malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Andre Villas-Boas amesema hatua hiyo ya kufungwa, kwake anaichukulia kama changamoto ya kufikiria mbele na kukabiliana na timu ngumu kama Man Utd hivyo ameahidi kufungua ukurasa mwingine wa kusaka ushindi kwa namna yoyote ile.

Chelsea watarejea tena uwanjani mwishoni mwa juma hili katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambapo watakua nyumbani Stamford Bridge wakiwakaribisha Swansea City lakini siku ya jumatano watacheza mchezo wa kuwnai kombe la ligi dhidi ya Fulham.

No comments:

Post a Comment