KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 19, 2011

MANCINI ASHANGAZA KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI.

Katika hali ya kushangaza meneja wa Man City Roberto Mancini amedai kwamba kikosi chake jana kilishindwa kushomoza na ushindi dhidi ya Fulham, kufuatia upungufu wa wachezaji alio nao kwa sasa.

Madai hayo ya Roberto Mancini yaliwashangaza wengi katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema asilimia kubwa ya wachezaji wake ni majeruhi hivyo hana budi kufikiria kufanya usajili katika kipindi cha dirisha dogo mwezi januari mwaka 2012 lakini inatakiwa ikumbukwe kuwa tayari Man city wameshatumia paund million 300 katika usajili baada ya kuwa chini ya Taykun kutoka Falme za kiarabu Sheikh Mansour bin Zayed bin Sultan Al Nahyan.

Amesema katika mpambano huo kikosi chake kiliwakosa wachezaji kama James Milner pamoja na Nigel de Jong ambao anaamini endapo wangekua na hali nzuri mambo yangekua safi ndani ya dakika 90.

Katika hatua nyingine meneja huyo kutoka nchini italia ameonyesha kukasirishwa na mwenendo wa wachezaji wake ambapo amedai walikuwa hawana sababu ya kushindwa kuwazui wapinzani wao ambao tayari walikua nyuma kwa idadi ya mabao mawili kwa sifuri hadi katika dakika ya 60 lakini mpaka mwishoni mwa mpambano huo ubao wa m ulisomeka mbili kwa mbili.

Hata hivyo amedia kwamba hatua hiyo imewafundisha namna ya kucheza kwa malengo katika michezo ijayo ambayo anaamini watafanya vyema kwa lengo la kutaka kutimiza mipango ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Mabao ya Man City katika mpambano huo yalipachikwa nyavuni na mshambuliaji kutoka nchini Argentina Sergio Aguero huku Bobby Zamora pamoja na Danny Murphy wakifunga mabao ya Fulham.

No comments:

Post a Comment