KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 22, 2011

Cesc Fabregas AIOKOA FC BARCELONA.

Bao lililofungwa na kiungo kutoka nchini humo Cesc Fabregas katika dakika ya 77, liliwaokoa mabingwa watetezi wa LA LIGA FC Barceloana kutopoteza mchezo wa kwanza wakiwa ugenini walipokua wakicheza na Valencia huko Stadio Mestella.

Cesc Fabregas alifunga bao hilo, baada ya fc Barcelona kuwa nyuma kwa idadi ya mabao mawili kwa moja ambapo wenyeji, Valencia walitangulia kupata bao la kuongoza katika dakika ya 12 baada ya beki kutoka nchini Ufaransa Eric Abidal kujifunga mwenyewe na dakika mbili baadae Barca walisawazisha kupitia kwa Pedro Rodríguez.

Katika dakika ya Valencia walijipatia bao la o la pili kupitia kwa Pablo Daniel Piatt baada ya kumiliki mpira kwa muda mrefu hali ambayo iliwachanganya Barcelona.

Matokeo ya michezo mingine iliyochezwa jana ni katika ligio ya nchini Hispania pamoja na:


Estadio La Rosaleda, Málaga
Málaga CF 1 - 0 Athletic Bilbao

Estadio Vicente Calderón, Madrid
Atlético Madrid 4 - 0 Sporting Gijón

Vallecas, Madrid
Rayo Vallecano 1 - 2 Levante UD

El Sardinero, Santander
Racing Santander 0 - 0 Real Madrid

Kwa matokeo hayo sasa Valencia wanaendelea kubaki kileleni mwa ligi ya nchini Hispania wakiwa na point 10, wakifuatiwa na Malaga wenye point 9, nafasi ya tat inakamatwa na Real Betis.

Barcelona anafuatia kwa kufikisha point 8 huku real Madrid wakikamata nafasi ya saba kwa kumiliki point 7.

Hii leo ligi hiyo inaendelea tena kwa michezo miwili ambapo:

Estadio Cornellá-El Prat, Cornellà deLlobregat
RCD Espanyol v Getafe CF

Estadio Benito Villamarin, Seville
Real Betis v Real Zaragoza

No comments:

Post a Comment