KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 22, 2011

Claudio Ranieri MENEJA MPYA INTER MILAN.



Aliekua meneja wa klabu ya Valencia, Chelsea pamoja na As Roma Claudio Ranieri ametangazwa kuwa mrithi wa kiti cha umeneja ndani ya klabu ya Inter Milan ya nchini Italia.
Claudio Ranieri ametajwa kuchukua nafasi hiyo baada ya uongozi wa Inter Milan kumtimua kazi Gian Piero Gasperini mara baada ya kushindwa kupata ushindi katika michezo mitatu ya mwanzoni mwa msimu huu huko nchini Italia pamoja na katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Trabzonspor.

Claudio Ranieri amesema amekubalia kujiunga na klabu hiyo kutokana na ubora na uziri uliopo ndani ya kikosi cha The Nerazzurri hivyo anaamini atafikia malengo yaliyowekwa na uongozi waliomuamini na kumpa mkataba wa mwaka mmoja ambao utaboresha endapo atafikia malengo mwishoni mwa msimu huu.

Amesema mipango mikubwa klabuni hapo ni kuhakikisha suala la ushindi linapewa kipaumbele, na kisha mengine yanafuata hatua ambayo amekiri itapatikana kutokana na ushirikiano kati yake na wachezaji, viongozi pamoja na mashabiki ambao amewaomba kukishabikia kikosi chao popote kitakapokwenda.

Claudio Ranieri pia akamzungumzi meneja alietimuliwa kazi huko Guissepe Meazza Gian Piero Gasperini kwa kusema bado ni meneja mzuri na kuondoka kwake klabuni hapo hakumaanishi yeye ana uwezo kuliko wengine bali alichokiona kwa meneja huyo mwenye umri wa miaka 53 ni utambulisho wa mfumo mpya ambao ulishindwa kueleweka mapema kwa wachezaji wa Inter Milan.

Claudio Ranieri ambae kwa mara ya mwisho alikinoa kikosi cha AS Roma kabla ya kujiuzulu mwanzoni mwa mwaka huu, ataanza kazi ya kukinoa kikosi cha Inter Milan mwishoni mwa juma hili dhidi ya Bologna na kisha atawajibika katika kibarua cha pili katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya CSKA Moscow watakaokua nyumbani huko nchini Urusi kati kati ya juma lijalo.

No comments:

Post a Comment