
Frank Lampard amesema alistahili kuendelea kubaki kikosini kwa ajili ya kuongeza purukushani za kusaidiana na wengine katika harakati za kusaka ushindi wakiwa ugenini lakini mwisho wa siku walijikuta wakilazimishwa sare ya bao moja kwa moja.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33, amesema kwamba mchezo wa jana ulikua mzuri sana kwake kutokana na uchezaji mzuri wa kikosi cha Chelsea ulioonyeshwa uwanjani na alidhani angemaliza katika dakika zote 90.
Hata hivyo amedai kwamba anaheshimu maamuzi ya meneja Andre Villas Boas ambae ndie mwenye jukumu la kuamua nani acheze tena kwa wakati gani na mchezo gani katika msimu mzima wa soka.

Andre Villas Boas amesema mashabiki wengi walikua wanambeza kiungo huyo kwa kisingizio cha kushikwa kwa kiwango chake ambapo anadhani hali hiyo ilitokana na kutompanga katika michezo kadhaa iliyopita.
Amesema hatua ya kufunga bao katika mpambano huo imekuwa nzuri kwake na pia imekuja kwa wakati muafaka baada ya kuwatahadharisha mashabiki wanaombeza Frank Lampard.
No comments:
Post a Comment